Tuesday, September 16, 2014

Sikika yafanya mkutano na Ofisi ya CAG Dodoma: 12 September 2014

Mkuu wa Programu za Sikika Bw. Patrick Kinemo (Kushoto) akiwakaribisha maofisa kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) mkoani Dodoma walipotembelea ofisi za Sikika Dodoma ili kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Sikika.
Mkuu wa Ofisi ya Kanda Sikika Dodoma Bi. Norah Mchaki akiwasilisha mada juu ya zoezi la Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) katika mkutano baina ya Sikika na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) mkoani Dodoma.
Bi. Norah Mchaki akiwasilisha mada. 


Mhasibu Msaidizi kanda ya kati kutoka ofisi ya NAOT Dodoma Bw. Mhina Kombo (Kulia) akiuliza swali juu ya zoezi la SAM linavyofanya kazi na (kushoto) ni Mkaguzi Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma Bw. Martin Madalo.
 Bw. Mhina Kombo (Kulia) akifafanua jambo.
Wakaguzi wa vituo kutoka Ofisi ya NAOT Dodoma Kulia ni Bw. Fredrick Magawa na Bw. George Yohana katika ofisi za Sikika Dodoma.

Bi. Norah Mchaki akieleza Sikika inavyofanya zoezi la SAM linavyofanya kazi katika wilaya ambazo Sikika inafanya kazi.
Picha ya Pamoja: Sikika na NAOT  Dodoma.

Post a Comment