Friday, September 18, 2015

Mkutano wa Wadau Kujadili Upatikanaji wa Dawa Muhimu na Vifaa tiba nchini na Changamoto zake.

Mkuu wa Idara ya Dawa na Vifaa tiba, Sikika Bi. Alice Monyo akifungua mkutano uliojumuisha Wadau mbalimbali nchini. Mkutano huo ulikua na lengo la kujadili changamoto, mapendekezo na maazimio ya pamoja juu ya mfumo wa usambazaji dawa muhimu na vifaa tiba nchini.   

Meneja wa Kanda Bohari ya Dawa (MSD) Dodoma Bw. John Sipendi akichangia juu changamoto za usambazaji wa dawa na vifaa tiba nchini. 

Kaimu Mganga Mkuu wilaya ya Ilala Dkt. Willy Sangu (Kulia) na Mganga mfawidhi zahanati ya Mongolandege, Rumishaeli Mwanga wakifuatilia mjadala.  
Kaimu Mganga Mkuu, wilaya ya Iramba, Bw. Sunday Alphonce (Kulia) akifuatilia mjadala.
Mfamasia kutoka wilaya ya Kondoa, Bw. Said Mayanja (Kushoto) na Kaimu Mganga mkuu wilaya ya  Kondoa, Reginald Saria (wa pili kushoto) walikuwa miongoni mwa washiriki.

Meneja wa Kanda Bohari ya Dawa (MSD) - Moshi, Bw. Celestine Hauli akichangia jambo katika mkutano huo. Kulia ni Mfamasia kutoka wilaya ya Temeke, Bw. Shaidi Simba. 
Afisa Programu, Sikika Bi. Josephine Nyonyi akiwasilisha mwenendo wa Bajeti ya dawa muhimu na vitaa tiba. Mganga Mkuu wilaya ya Kiteto, Dk. Sungwa Kabisi (Wa kwanza kushoto) na Mganga Mfawidhi zahanati ya Ndaleta - Kiteto Bw. Bahatieli William wakifuatilia mjadala.  
 Bi. Alice Monyo kutoka Sikika, akifanunua jambo.  
Bw. Celestine Hauli akitoa ufafanuzi juu ya tatizo la mfumo wa usambazaji dawa na vifaa tiba katika baadhi ya vituo vya huduma za afya vya umma nchini. 
Regional Prime Vender Coordinator - Mkoa wa Dodoama Dk. Ibenzi Ernest akitoa ufafanuzi. 
Mfamasia Manispaa ya Ilala, Bw. Moses Michael akipitia Jarida la Sikika. 
 Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) Bi. Alambo Msusa akipitia baadhi ya nyaraka. 
Afisa Programu, Sikika Bi. Scholastica Lucas akiwasilisha mada juu ya changamoto za mfumo wa usambazaji wa dawa muhimu na vifaa tiba nchini. 

Kaimu Mganga Mkuu, Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Sigfrid Ishengoma akiishukuru Sikika juu ya ufuatiliaji na kuibua changamoto za mfumo wa usambazaji dawa muhimu na vifaa tiba.  

Dk. Mfuko akitoa ufafanuzi juu ya mfumo wa usambazaji dawa.  

Baadhi ya wadau wakiwa katika majadiliano. 
Mganga Mfawidhi  wilaya ya Temeke, Bi. Batuli Luhanda akitoa mapendekezo jinsi ya kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba  katika ngazi zote nchini. 


Mfamasia wa Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Paulo Ngoile akipendekeza Serikali itekeleze Azimio la Abuja.
Mganga Mkuu wilaya ya Singida Vijijini, Dkt. Erick Bakuza akichangia mada juu ya kuboresha mfumo wa upatikanaji dawa na vifaa tiba  katika ngazi zote. 
Afisa kutoka NHIF wilaya ya Kibaha, Bw. Evance Nyangasi  akitoa ufafanuzi juu ya Mfuko  wa Bima ya Afya. 
Bw. John Sipendi akitoa mapendekezo juu ya uboreshaji wa mfumo huo.  
Baadhi ya Wadau wa masuala ya dawa na vifaa tiba nchini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo. 

Post a Comment