Wednesday, November 9, 2016

Ziara ya Timu ya SAM Kondoa kutathmini hali ya vituo vya afya na zahanati wilayani humo

Jengo zuri la zahanati ya Mkekena, wilayani Kondoa ambalo pia limejengewa sehemu maalum ya kupitia watu wenye mahitaji maalumu (Walemavu na Wazee). Hata hivyo, choo chake  (pichani chini) hakiendani na hadhi ya jengo hilo.

Dawa zikiwa zimehifadhiwa juu ya kitanda  katika zahanati ya Mkekena kutokana na upungufu wa samani.
Wajumbe wa timu ya SAM walikagua wodi ya wanawake katika kituo cha afya Mnenia. Jengo hilo halitumiki kwa muda mrefu kutokana na kutokuwa na vifaa vya kutosha kama magodoro na vitanda. 
Baadhi ya vitanda katika wodi hiyo vikiwa havina magodoro. 
Kizimba cha kuchomea taka hatarishi katika kituo cha Mnenia ambacho hakijatumika kwa zaidi ya miaka 10 kutokana na kukosa fedha za ukarabati.  
Shimo linalotumika kuchomea taka hatarishi - Mnenia 

Mfano mzuri wa miundombinu rafiki kwa watu wenye mahitaji maalumu (walemavu na wazee) - Mnenia. 
 Choo kipya katika zahanati ya Baura  ambacho hakitumiki kutokana na tatizo la ukosefu wa maji, badala yake  wagonjwa kutumia choo cha muda (pichani chini). 

Ukosefu wa samani: Chumba cha kuhifadhia dawa katika zahanati ya Baura. 
Wajumbe wa timu ya SAM (Kondoa) wakitoka kukagua ujenzi wa jengo la nyumba ya watumishi - Baura. 
Sanduku la kutolea maoni (Baura). 
(Pichani Juu) Jengo zuri la zahanati ya Bolisa, (chini) choo cha zahanati hiyo ambacho kina nyufa ndani hivyo kusababisha wagonjwa kushindwa kukitumia. 

(Juu) Shimo la choo limeanza kuchimbwa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa choo kipya.
Ubao wa matangazo - Bolisa. 
Jengo la zahanati ya Hachwi (Kondoa) ambalo halijawahi kutumika tangu mwaka 2007 ujenzi wake ulipokamilika. Ujenzi wake ulianza mwaka 2005 kwa nguvu za wananchi na ulikamilishwa mwaka 2007 na mfadhili kutoka Uholanzi. Hata hivyo, jengo hilo halina choo,  maji wala meme. 

(Juu) Kitanda cha kuzalishia akina mama wajawazito katika zahanati ya Hachwi. 

Wajumbe wa timu ya SAM wakikagua choo cha zahanati ya Hachwi ambacho paa lake liliezuliwa na upepo. 

           
 Viongozi wa kijiji cha Mongolo na timu ya SAM (Kondoa) wakikagua ujenzi wa zahanati ya Mongolo ambao kwa zaidi ya miaka 20 haujakamilika kutokana na mgogoro kati ya wananchi na uongozi wa halmashauri ya Kondoa. Mgogoro huo ulijitokeza baada ya halmashauri hiyo kushauri kuvunjwa kwa jengo hilo na kutaka itumike ramani mpya badala ya  ile ya zamani. Ujenzi huo ulianza mwaka 1994 kwa nguvu za wananchi hadi kufikia hatua ya lenta. 
Jengo la zahanati ya Mongolo ambalo halijakamilika ujenzi tangu mwaka 1994.             
Muonekano wa jengo la zahanati ya Masange ( kwa nje). Chini: Hali ya jengo hilo kwa ndani si ya kuridhisha kutokana na kuwa na nyufa nyingi, ubovu wa dari hali inayohatarisha maisha ya watumiaji wakiwemo wagonjwa.
Kitanda cha uchunguzi kwa wagonjwa ambacho pia hutumika kwa ajili ya akina mama kujifungulia.


Timu ya SAM ikikagua ubora wa choo cha Masange. 
Chumba maalum cha kuhifadhia dawa - Masange.


Kitanda cha kujifungulia akina mama katika kituo cha afya Kisese (Kondoa), kimechakaa.Baadhi ya vifaa vinavyotumika kwa ajili ya mama wajawazito kujifungulia.


Kizimba cha kuchomea taka hatarishi ambacho ni kibovu, hivyo kutotumika kwa muda mrefu. Badala yake wanatumia shimo kutupia taka hizo kama inavyooneka katika picha (chini).

Post a Comment