Thursday, November 8, 2012

Mkutano wa Wadau wa Ugavi na Usambazaji wa Dawa na VIfaa Tiba - Tanzania 6 Novemba, 2012 Golden Tulip Hotel

Mkuu wa Idara ya dawa na vifaa tiba kutoka Shirika la Sikika,  PatrickKinemo akifungua mkutano wa wadau wa ugavi na usambazaji dawa na vifaa tiba Tanzania. Lengo kuu likiwa ni kutathmini changamoto za kimfumo wa ugavi na usambazaji dawa katika vituo vya umma.

Kikundi cha kinachowakilisha wananchi(watumiaji huduma za afya) wakijadili baadhi ya changamoto zinawakabili pindi wanapokuwa wanaenda kupata huduma za afya hospitalini.

Baadhi ya wadau kutoka Wizarani, Wafadhali na Waganga wakuu wakijadili kwa makini changamoto zinatokea katika usambazaji wa dawa na vifaa tiba Tanzania katika mkutano huo.

Mdau akichangia mapendekezo ya mfumo wa usambazaji dawa na vifaa tiba ili kuondokana  na kero za malalamiko ya kutokwepo kwa dawa na vifaa tiba katika baadhi ya vituo vya afya vya umma hapa nchini.

Wadau kutoka Bohari kuu ya dawa (MSD)  na Wizara wakitathmini jambo.

Karim Magimba akiwakilisha kikundi cha wananchi yaani watumiaji huduma za afya katika kueleza umuhimu wa mkutano huo ulivyowapa fursa pekee ya kuwasemea wananchi wenzao matatizo wanayakumbana nayo katika kupata huduma za afya.

Mfamasia Sophia Josaphat Bitta kutoka wilaya ya Kinondoni akielezea umuhimu wa mkutano wa wadau wa ugavi na usambazaji dawa na vifaa tiba ulivyompa fursa ya kuelezea changamoto wanazokutana nazo. 

Maria Sarungi Tsehai akiendesha mkutano huo kwa makini.

Wadau kutoka sehemu mbalimbali wakitathmini changamoto zao za kimfumo kwa pamoja .

Mdau akiwasilisha changamoto pamoja na mapendekezo katika mfumo wa usambazaji dawa na vifaa tiba nchini.

Patrick Kinemo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo. 

Wadau wakilisikiliza kwa makini mawasilisho ya changomoto, mapendekezo na maazimio ndani ya mkutano huo.






Changamoto na mapendekezo yalikua mengi kila kikundi kilipata fursa ya kipekee  katika kuwasilisha kabla ya maazimio waliyoafikia ndani ya mkutano katika kuboresha mfumo wa usambazaji na dawa na vifaa tiba Tanzania.

No comments: