Wednesday, July 11, 2018

Tumesitisha kuweka taarifa mpya kwenye blogu ya sikika-tz.blogspot.com

Tunasikitika kukutaarifu kwamba tumelazimika kufunga kwa muda Blog yetu ya www.sikika-tz.blogspot.com kutokana na  Kanuni za Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA)  na Maudhui ya Habari za Mtandaoni (2018), Kanuni ya 18 ambayo inaelekeza kuwa ni kosa  kisheria kutoa huduma za maudhui mtandaoni (Blogu, Majukwaa mtandaoni-Online forums, redio na televisheni mtandaoni) bila kusajiliwa na kupewa leseni kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania- TCRA. 

Tumesitisha kwa muda Blog yetu hadi tutakapopata mwongozo au maelezo ya kina hususan kuhusu kusajili na kulipia Blogu ya Sikika kwa vile haiingizi kipato chochote na pia haipo kibiashara bali ni kwa ajili ya kutoa taarifa muhimu kuhusiana na kazi za Sikika na wadau wake katika masuala ya Afya na Usimamizi wa matumizi ya fedha za umma. 

Kwa sasa unaweza kuendelea kupata taarifa za kazi zetu kupita website yetu ya www.sikika.or.tz na kwenye mitandao ya kijamii ifuatayo: 
  1. Twitter: @sikika1
  2. Ukurasa wa Facebook: sikika1
  3. Instragram: SikikaTanzania
  4. Youtube: SikikaTanzania 


Wednesday, April 25, 2018

Sikika yashiriki katika Uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu 2017

Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu nchini (LHRC), Bi. Helen Kijo Bisimba (Kushoto) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi. Katarina Rangitt wakikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Ripoti ya Haki za Binadamu kwa mwaka 2017. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa na ongezeko kubwa la ukiukwaji wa haki nchini. Haki 5 zilizovunjwa zaidi mwaka 2017 ni Haki ya Kuishi, Haki dhidi ya Ukatili, Haki ya na Usalama wa Mtu, Uhuru wa Kujieleza, Uhuru wa kukusanyika na Uhuru wa Kujumuika. #HumanRightsReport

Afisa Utafiti kutoka Kituo cha Haki za Binadamu Bw. Fundikila Wazambi akiwasilisha utafiti  wa ripoti hiyo kwa wadau mbalimbali wa Haki za Binadamu nchini.







Mkurugenzi wa Hodari Tanzania Bi. Imelda Lulu Urio akielezea juu Haki ya kuwa Huru na Usalama wa Mtu (Uuaji, Utekaji na Uteswaji unaofanywa na 'watu wasiojulikana'). 
Rais wa Chama cha Wanasheria - Tanganyika  Law Society (TLS), Bi. Fatma Karume akielezea hatari iliyopo kwa Watanzania kuendelea kukosa haki ya uwakilishi kisheria kutokana na uchache wa mawakili. Takwimu zinaonyesha kuwa wakili mmoja anahudumia wananchi 25,000.  
Bi. Jane  Magigita akizungumzia juu ya masuala ya Ukiukwaji wa Haki za Wanawake, Usawa wa Kijinsia na Kutobaguliwa.
Mkurungezi wa Sikika, Bw. Irenei Kiria 
akizungumzia Haki za Binadamu kwa upande wa sekta ya afya nchini. Kwa upande wa Haki Afya, ripoti hiyo inaonyesha kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwemo changamoto ya upungufu wa bajeti, vitanda, rasilimali watu, madawa na vifaa tiba. 

Mwanachama wa TAMASHA, Shirika la kuendeleza Haki za Vijana Bw. Richard Mabala akielezea juu ukiukwaji wa Haki za Watoto hususan katika upande wa elimu. 

Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Bi. Mishi Singano akichangia mada mara baada ya uwasilishwaji wa ripoti hiyo. 
Baadhi ya wanaharakati kutoka taasisi mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja. 

Thursday, March 22, 2018

Kigoma Ujiji LGA responds to Citizens’ plea

In 2017, Sikika facilitated a Social Accountability Monitoring (SAM) exercise in Kigoma Ujiji. As part of the exercise, during health facilities’ field monitoring visit, SAM team members identified several poorly constructed incinerators and placenta pits at Gungu health center and other facilities. They shared their findings with the local government authority during the stakeholders’ feedback meeting. Their main concern was on the absence of the required, up to standard placenta pits and the low quality of the incinerator constructed, taking into account that the taxpayers’ money was already spent and documented in the official district implementation reports.




Responding to SAM team’s findings, the service providers (Local Government Authority LGA) agreed to rectify the problem at Gungu health center. They commissioned a contractor to repair the said incinerator, dig the ash-pit that was not there and fencing it. However, during the construction of a placenta pit, the citizens noticed that what was being built was once again, below the required standards. The citizens decided to write a letter to Sikika and their local leaders, expressing their concerns and dissatisfaction.


Sikika commends the citizens for playing their role actively by monitoring how the public funds are spent to realize value for money. We also applaud the Kigoma Ujiji’s CHMT for their quick response; taking corrective measures after receiving the citizens’ complaint. The renovation of a new incinerator and extension of ash-pit is now ongoing.