Ripoti ya hivi karibuni kwa vyombo vya habari, imebainisha kuwa Rais wa
Tanzania, Jakaya Kikwete, wakati alipofanya ziara katika mkoa wa
Shandong nchini China, aliishukuru serikali ya nchi hiyo kujitolea
madaktari wake wafanyakazi nchini Tanzania kwa miaka 46 iliyopita.
Rais pia, alitumia nafasi hiyo kuelezea upungufu wa madaktari uliopo
nchini na kuiomba serikali ya China iendelea kusaidia madaktari
wanaojitolea ili kukabiliana na upungufu uliopo.
Kama hiyo haitoshi katika wiki hiyo hiyo, vyombo vya habari vilimnukuu
Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
akisema kuwa, serikali inapitia upya sera yake ya uajiri ili kuweza
kuwaajiri moja kwa moja wahitimu wa kada mbalimbali za afya wenye sifa,
baada ya kuhitimu masomo yao badala ya kusubiri watume maombi Wizarani.
Licha ya kwamba lilikuwa ni jambo jema kwa Rais kuishukuru serikali ya
China kwa msaada wake. Lakini, wakati umefika kwa serikali kuwekeza
zaidi kwa madaktari waliopo nchini, kwa kutekeleza mipango iliyopo ya
kukabiliana na upungufu wa madaktari, ukiwemo ule uliopendekezwa na
Mkurugenzi wa Mafunzo wa Wizara ya Afya.
Hakuna ubishi kuwa, Tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa wafanyakazi wa sekta ya afya wakiwemo madaktari.
Takwimu za hivi karibuni kutoka katika ripoti ya ufuatiliaji wa
utekelezaji wa Mpango Mkakati Sekta ya Afya ( MTR - HSSP III, 2013 )
unaonesha kuwa, Tanzania ina madaktari 0.5 kwa kila watu 10,000. Kiwango
cha chini kabisa kinachokubalika na Shirika la Afya Duniani (WHO) ni
angalau madaktari wawili kwa kila watu 10,000.
Licha ya uhaba huu, taarifa zinaonesha kwamba Tanzania ina idadi kubwa
ya madaktari wenye sifa, ambao hawafanyi kazi za utabibu kutokana na
sababu mbalimbali, ikiwemo kukosekana kwa mpango mzuri wa kuhakikisha
madaktari wote wanaohitimu wanaingia ama kuajiriwa katika utumishi wa
umma.
Mwaka 2012, Sikika ikishirikiana na Chama cha Madaktari Tanzania ( MAT )
walifanya utafiti ili kubaini walipo madaktari. Matokeo ya utafiti huo,
yalionesha kuwa takribani asilimia 40 ya madaktari hawafanyi kazi ya
udaktari waliyoisomea; kwa maana nyingine, hawafanyi kazi za kutibu
wagonjwa hospitalini.
Wengi wanafanya kazi ambazo si za kitabibu katika taasisi mbalimbali
zisizo za kiserikali na wengine huamua kuacha kazi yao ya udaktari na
kufanya kazi nyingine kama Mkurugenzi wa Mafunzo, Wizara ya Afya
alivyonukuliwa na vyombo vya habari.
Uamuzi wa kuleta madaktari kutoka nje, si tu kwamba ni suluhisho la muda
mfupi katika kutatua tatizo la upungufu, lakini pia kwa kiasi kikubwa
kunaathiri matumizi ya kiasi kidogo cha fedha kilichopo, ambacho
kingeweza kutumika katika kuwaajiri na kuwavutia madaktari katika
utumishi wa umma.
Madaktari kutoka nje, hata kama ni wa kujitolea, huambatana na gharama nyingine ambazo kimsingi hugharamiwa na nchi inayowachukua.Gharama hizi zaweza kuwa ni pamoja na malazi, tiketi za ndege, usafiri ndani ya nchi, chakula na mafunzo ya lugha ya Kiswahili, ambazo kwa ujumla wake zinaweza kuwa ni kiasi kikubwa cha fedha.
Ukiangalia vitabu vya bajeti na Mipango ya Matumizi ya Muda wa Kati ya mwaka 2012/13 na 2013/14 kwa mfano, gharama za kumhudumia daktari mmoja kutoka nje ni kati ya Sh. 2,000,000 – 5,000,000. Zaidi, madaktari hawa kimsingi hupelekwa katika hospitali za mikoa ama za rufaa badala ya zahanati na vituo vya afya vilivyopo vijijini ambako ndio kuna mahitaji makubwa ya watoa huduma za afya.
Tatizo la upungufu wa wafanyakazi katika sekta ya afya, kama ilivyoelezwa hapo mwanzo, linachangiwa na sababu mbalimbali, zikiwemo mazingira magumu ya kazi, kucheleweshwa ama kutokulipwa mapunjo ya mishahara, kucheleweshwa mishahara kwa wafanyakazi wapya na kuchelewa kupandishwa vyeo.
Haya yote yaweza kuwa ni dalili za kukosekana kwa uratibu mzuri miongoni mwa wizara husika, wakati wa kuandaa mipango na bajeti kwa ajili ya kuajiri na kusambaza wafanyakazi wa sekta ya afya. , na ni moja ya changamoto zilizotajwa katika ripoti ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mpango mkakati wa III wa wizara ya afya na ustawi wa jamii ( MTR _ HSSP III, 2013 ).
Wizara hizo ni pamoja na Wizara ya Fedha yenye mamlaka ya kutenga bajeti kwa ajili ya kuajiri na kusambaza mishahara, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma yenye mamlaka ya kutoa idadi ya nafasi na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo huajiri na kusambaza waajiriwa kwa idadi iliyoruhusiwa na Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma, na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambayo huomba nafasi za waajiriwa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Ni muhimu pia, Wizara ikabainisha changamoto nyingine mbalimbali, kama zilizobainishwa na Mkurugenzi wa Mafunzo, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Muda mrefu unaopita baada ya wahudumu wa afya kuhitimu masomo na kutuma maombi ya kazi.
Pia muda mrefu unaotumika kukamilisha zoezi la ajira na kusambaza wafanyakazi hutengeneza mianya ya wahitimu wa afya wenye sifa kutafuta ajira mbadala, ambazo zaweza kuwa nje ya sekta ya afya. Sikika inafurahia wazo la kupitia mchakato wa ajira wenye lengo la kupata ufumbuzi wa changamoto zilizoainishwa na ingependa kuona mapitio kama haya yanafanyika kwenye maeneo mengine ili kutatua changamoto zilizotajwa katika makala haya.
Tunatoa wito kwa Serikali, kuanza kushughulikia tatizo la upungufu wa wafanyakazi katika sekta ya afya nchini kwa kulenga kupata ufumbuzi wa ndani kwanza. Ni busara kushughulikia mambo ambayo ni kikwazo cha kuwaingiza wafanyakazi wa sekta ya afya, wakiwemo madaktari katika mifumo ya umma badala ya kuendelea na utegemezi katika ufumbuzi wa muda kama huu wa kuchukua madaktari wa kigeni.

Makala hii imechapishwa na Gazeti la: NIPASHE tarehe 18 Novemba, 2014

No comments:
Post a Comment