Tuesday, April 14, 2015

MAOMBI YA KUKUSIHI KUTO KUTIA SAINI MISWADA YA SHERIA YA TAKWIMU YA 2015 NA SHERIA YA MAKOSA YA MITANDAO BILA KUFANYIWA MAREKEBISHO


Mhe. Rais, Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania, ni muungano wa mashirika zaidi ya 100 yanayo tetea haki za binadamu Tanzania. Mtandao kwa kushirikiana na Wanachama wake pamoja na wasio wanachama tumehuzunishwa na kitendo cha Bunge la Jamhuri ya Muungano kupitisha Muswada wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 na Muswaada wa Sheria ya Makosa ya Mtandaoni bila kuviondoa vifungu vinavyokwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Haki za Binadamu kwa Ujumla.

Tunafahamu kabisa dhamira yako ya kuhakishia watanzania wanapata uhuru wa maoni na uhuru wa kufanya shughuli zenye tija kwa Taifa kwa uhuru. Pia tunatumia fursa hii kukupongeza Mhe. Rais Kw kwa jitihada za kuongeza wigo wa ushiriki wa wadau katika mambo mbalimbali kwa kuanzisha progamu mbalimbali za utawala bora, uwazi na ukweli kama vile Open Government Partnership na mengineyo. Kwa misingi hiyo Mheshimiwa Rais, tunashauri kabla ya kutia saini miswaada hii upate muda wa kusikiliza kilio cha jamii juu ya ubaya wa sheria hizi kwa mustakabali wa Taifa. Sheria Hizi zikitumika katika utwawala wako zitatia shaka dhamira yako nzuri ambayo umekuwa ukisimamia toka uingie madarakani ya kuongeza wigo na uhuru wa habari na ushiriki wa wadau katika maendeleo ya kitaifa.  

Soma zaidi...Sikika

No comments: