| Dawa zikiwa zimehifadhiwa juu ya kitanda katika zahanati ya Mkekena kutokana na upungufu wa samani. |
| Wajumbe wa timu ya SAM walikagua wodi ya wanawake katika kituo cha afya Mnenia. Jengo hilo halitumiki kwa muda mrefu kutokana na kutokuwa na vifaa vya kutosha kama magodoro na vitanda. |
| Baadhi ya vitanda katika wodi hiyo vikiwa havina magodoro. |
| Kizimba cha kuchomea taka hatarishi katika kituo cha Mnenia ambacho hakijatumika kwa zaidi ya miaka 10 kutokana na kukosa fedha za ukarabati. |
| Shimo linalotumika kuchomea taka hatarishi - Mnenia |
| Mfano mzuri wa miundombinu rafiki kwa watu wenye mahitaji maalumu (walemavu na wazee) - Mnenia. |
| Choo kipya katika zahanati ya Baura ambacho hakitumiki kutokana na tatizo la ukosefu wa maji, badala yake wagonjwa kutumia choo cha muda (pichani chini). |
| Ukosefu wa samani: Chumba cha kuhifadhia dawa katika zahanati ya Baura. |
| Wajumbe wa timu ya SAM (Kondoa) wakitoka kukagua ujenzi wa jengo la nyumba ya watumishi - Baura. |
| Sanduku la kutolea maoni (Baura). |
| (Pichani Juu) Jengo zuri la zahanati ya Bolisa, (chini) choo cha zahanati hiyo ambacho kina nyufa ndani hivyo kusababisha wagonjwa kushindwa kukitumia. |
| (Juu) Shimo la choo limeanza kuchimbwa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa choo kipya. |
| Ubao wa matangazo - Bolisa. |
Jengo la zahanati ya Hachwi (Kondoa) ambalo halijawahi kutumika tangu mwaka 2007 ujenzi wake ulipokamilika. Ujenzi wake ulianza mwaka 2005 kwa nguvu za wananchi na ulikamilishwa mwaka 2007 na mfadhili kutoka Uholanzi. Hata hivyo, jengo hilo halina choo, maji wala meme.
| (Juu) Kitanda cha kuzalishia akina mama wajawazito katika zahanati ya Hachwi. |
| Wajumbe wa timu ya SAM wakikagua choo cha zahanati ya Hachwi ambacho paa lake liliezuliwa na upepo. |
| Jengo la zahanati ya Mongolo ambalo halijakamilika ujenzi tangu mwaka 1994. |
No comments:
Post a Comment