Wednesday, April 25, 2018

Sikika yashiriki katika Uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu 2017

Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu nchini (LHRC), Bi. Helen Kijo Bisimba (Kushoto) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi. Katarina Rangitt wakikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Ripoti ya Haki za Binadamu kwa mwaka 2017. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa na ongezeko kubwa la ukiukwaji wa haki nchini. Haki 5 zilizovunjwa zaidi mwaka 2017 ni Haki ya Kuishi, Haki dhidi ya Ukatili, Haki ya na Usalama wa Mtu, Uhuru wa Kujieleza, Uhuru wa kukusanyika na Uhuru wa Kujumuika. #HumanRightsReport

Afisa Utafiti kutoka Kituo cha Haki za Binadamu Bw. Fundikila Wazambi akiwasilisha utafiti  wa ripoti hiyo kwa wadau mbalimbali wa Haki za Binadamu nchini.







Mkurugenzi wa Hodari Tanzania Bi. Imelda Lulu Urio akielezea juu Haki ya kuwa Huru na Usalama wa Mtu (Uuaji, Utekaji na Uteswaji unaofanywa na 'watu wasiojulikana'). 
Rais wa Chama cha Wanasheria - Tanganyika  Law Society (TLS), Bi. Fatma Karume akielezea hatari iliyopo kwa Watanzania kuendelea kukosa haki ya uwakilishi kisheria kutokana na uchache wa mawakili. Takwimu zinaonyesha kuwa wakili mmoja anahudumia wananchi 25,000.  
Bi. Jane  Magigita akizungumzia juu ya masuala ya Ukiukwaji wa Haki za Wanawake, Usawa wa Kijinsia na Kutobaguliwa.
Mkurungezi wa Sikika, Bw. Irenei Kiria 
akizungumzia Haki za Binadamu kwa upande wa sekta ya afya nchini. Kwa upande wa Haki Afya, ripoti hiyo inaonyesha kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwemo changamoto ya upungufu wa bajeti, vitanda, rasilimali watu, madawa na vifaa tiba. 

Mwanachama wa TAMASHA, Shirika la kuendeleza Haki za Vijana Bw. Richard Mabala akielezea juu ukiukwaji wa Haki za Watoto hususan katika upande wa elimu. 

Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Bi. Mishi Singano akichangia mada mara baada ya uwasilishwaji wa ripoti hiyo. 
Baadhi ya wanaharakati kutoka taasisi mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja. 

No comments: