Tunasikitika kukutaarifu kwamba tumelazimika kufunga kwa muda Blog yetu ya www.sikika-tz.blogspot.com kutokana na Kanuni za Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) na Maudhui ya Habari za Mtandaoni (2018), Kanuni ya 18 ambayo inaelekeza kuwa ni kosa kisheria kutoa huduma za maudhui mtandaoni (Blogu, Majukwaa mtandaoni-Online forums, redio na televisheni mtandaoni) bila kusajiliwa na kupewa leseni kutoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania- TCRA.
Tumesitisha kwa muda Blog yetu hadi tutakapopata mwongozo au maelezo ya kina hususan kuhusu kusajili na kulipia Blogu ya Sikika kwa vile haiingizi kipato chochote na pia haipo kibiashara bali ni kwa ajili ya kutoa taarifa muhimu kuhusiana na kazi za Sikika na wadau wake katika masuala ya Afya na Usimamizi wa matumizi ya fedha za umma.
Kwa sasa unaweza kuendelea kupata taarifa za kazi zetu kupita website yetu ya www.sikika.or.tz na kwenye mitandao ya kijamii ifuatayo:
- Twitter: @sikika1
- Ukurasa wa Facebook: sikika1
- Instragram: SikikaTanzania
- Youtube: SikikaTanzania
No comments:
Post a Comment