Wednesday, March 27, 2013

Sikika ikiendesha mafunzo ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji wa Jamii (Social Accountability Monitoring -SAM) katika wilaya 5 za Kondoa, Kiteto, Mpwapwa, Singida Vijijini na Iramba kwa lengo la kufuatilia uwajibikaji katika sekta ya afya.

Baadhi ya wajumbe wa timu ya SAM wilayani Iramba wakikusanya taarifa katika moja ya ziara za kuhakiki miradi ya maendeleo ya Afya.


Mkuu wa wilaya ya Iramba Mh. Yahya Nawanda akisisitiza uwajibikaji wa watendaji wa halmashauri na madiwani kwa wananchi wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wadau yaliyofanywa na Sikika wilayani humo.


Ubao wa matangazo ukiwa umehifadhiwa ndani ya ofisi ya Mganga mfawidhi badala ya nje.




Mwananchi wilayani Kiteto akijaribu kujinyoosha ili afikie  sanduku la maoni ambalo limewekwa juu,  mahali ambapo wananchi wengi hawawezi kulifikia.


 Shimo la takataka kwenye moja ya zahanati wilayani Singida, linatotumika badala ya kizimba maalumu.


Baadhi ya wajumbe wa timu ya SAM wakiwa katika majadiliano wilayani Kondoa

No comments: