Muungano wa Asasi za Kiraia Tanzania umeandaa Mdahalo wa wazi
kuhusu Changamoto za Mchakato wa Katiba mpya.
Mdahalo huo utafanyika tarehe 31 /5/2014 katika Ukumbi wa Blue
Pearl Hotel, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa
10.00 Jioni.
Mdahalo huo utatangazwa moja kwa moja na vituo vya ITV, ABM Radio ya Dodoma, pamoja na Chuchu FM na Istiqama Radio za Zanzibar.
Vyombo vingine vya habari vitakavyopenda kuutangaza Mdahalo
huu kwa maslahi ya umma pia vinakaribishwa.
Watoa Mada ni waliokuwa wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba: Prof. Mwesiga
Baregu na Bw. Awadhi Ally Saidi.
Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki katika mdahalo huu ili
kuhakikisha kuwa Tanzania inapata katiba mpya inayokidhi maslahi ya watanzania.
Wote Mnakaribishwa !!!
No comments:
Post a Comment