UKOSEFU wa mara kwa mara wa dawa muhimu na vifaa tiba katika
vituo vya huduma za afya vya umma bado ni tatizo Tanzania. Tatizo hili
linachangia kutolewa kwa huduma duni za afya zinazopelekea athari kwa afya za
wananchi.
Tathmini mbalimbali zimeonesha kuwa upatikanaji wa dawa
muhimu na vifaa tiba ni mdogo katika vituo vya huduma za afya vya umma. Kwa
mfano, utafiti uliofanywa na Sikika mwaka 2012 umeonesha kuwa asilimia 52 ya
hospitali [N=52] hazikuwa na dawa muhimu na vifaa tiba kwa zaidi ya wiki nne.
Moja ya sababu kuu za kukosekana kwa dawa muhimu na vifaa tiba ni bajeti ndogo inayotengwa na serikali.
Mwenendo wa mgao wa fedha za dawa muhimu na vifaa tiba kutoka Bajeti ya
WAUJ kutoka 2008/09 hadi 2014/15
Mwaka
|
Bajeti ya WAUJ (Tsh Bilioni)
|
Bajeti
ya dawa muhimu na vifaa tiba (Tsh Bilioni)
|
Mabadiliko
ya asilimia ya bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba
|
|
2008/09
|
440.2
|
53.4
|
||
2009/10
|
478.9
|
49.6
|
-7.1
|
|
2010/11
|
676.3
|
61.4
|
23.8
|
|
2011/12
|
584.2
|
78.7
|
28.2
|
|
2012/13
|
576.1
|
80.5
|
2.3
|
|
2013/14
|
753.9
|
64
|
-20.5
|
|
2014/15
|
622.9
|
45.8
|
-28.4
|
Chanzo: Sikika 2010/2011 Health Sector Budget Analysis, Sikika Budget Analysis of the MoHSW for fiscal year 2013/14.
Mahitaji ya dawa
muhimu na vifaa tiba
Ingawa mojawapo ya vipaumbele vya Wizara ya Afya ni kuboresha
upatikanaji wa dawa muhimu, mgao wa fedha kwa dawa muhimu na vifaa tiba umekuwa
hauendani na mahitaji yake. Kwa mfano kwa mujibu wa makadirio ya Wizara ya Afya zitahitajika
kiasi cha Tsh 250 bilioni kukidhi mahitaji ya dawa muhimu kwa mwaka wa fedha
2014/15. Hata hivyo, mgao unaotarajiwa kupangwa ni shilingi bilioni 45 tu. Mgao
huu ni sawa na asilimia 7.7 ya mahitaji.
Pamoja na hivyo, ingawa kipaumbele cha Wizara ya Afya ni
kupungunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na kujifungua, bajeti ya vifaa vya
kujifungulia (delivery kits) inapungua mwaka hadi mwaka. Mfano, kwa mwaka wa
fedha 2012/13 zilitengwa jumla ya Tsh bilioni nne kwa ajili ya vifaa vya
kujifungulia. Bajeti hii ilipungua kufikia bilioni tatu mwaka 2013/14, na kama
hakutakuwepo mabadiliko itapungua hadi kufikia shilingi bilioni moja na nusu
mwaka ujao wa fedha 2014/15
Pia, pamoja na serikali kuahidi bunge mwaka jana kulipa deni
ambalo MSD inaidai serikali, deni hilo limeongezeka toka shilingi bilioni 76
mwaka 2013 hadi bilioni 89 mwaka 2014
Mjadala wa Bunge juu
ya Bajeti ya WAUJ
Mapendekezo
1. Serikali
itafute fedha za ziada kutoka katika sekta nyingine (kuhamisha) ili kuongeza
bajeti ya dawa muhimu inayotarajiwa kutengwa kwa mwaka wa fedha 2014/15 kutoka
bilioni 45 hadi bilioni 250 (kwa mujibu wa makadirio ya Wizara ya Afya)
2. Wizara
ya Afya na ustawi wa Jamii ihamishe fedha kutoka kwenye idara nyingine kwenda
kwenye dawa muhimu na vifaa tiba ili kuweza kuwa na bajeti inayolingana na
mahitaji.
3. Serikali
ijadiliane na wafadhili ili waweze kuongeza fedha katika bajeti hii ya mwaka
2014/15 (kama suluhisho la muda mfupi) wakati ikiendelea kubainisha
suluhisho la kudumu kama kuboresha na kusimamia ukusanyaji wa kodi, kupunguza
au kuondoa misamaha ya kodi pia kuboresha makusanyo yannayokana na mifuko ya
afya kama Mfuko wa Afya wa jamii(CHF) na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa.(NHIF).
Serikali inapaswa kuwa Mchangiaji mkuu wa dawa muhimu na vifaa tiba na sio
kuwaachia jukumu hili wafadhili.
4. Mipango
na mgao wa bajeti unapaswa kuzingatia
mapendekezo yaliyotolewa na bunge kupitia kamati ya kudumu ya huduma za
jamii.
Mr. Irenei Kiria
Executive Director of Sikika, P.O. Box 12183 Dar es
Salaam,
Tel: +255 222 666355/57, Fax: 2668015, Email:
info@sikika.or.tz, Website: www.sikika.or.tz
No comments:
Post a Comment