Wednesday, June 18, 2014

Mratibu Sikika wilayani Kondoa Bw. Nelson Lema alipotembelea Zahanati/Vituo vya Afya vya Thawi, Chololo, Mnenia na Sakami juu ya Upatikanaji wa Huduma za Afya

Kaimu Afisa Mtendaji wa kata ya Thawi  Ibrahimu Kisuju akizungumza na baadhi ya wajumbe wa timu ya SAM walipotembelea zahanati ya Thawi wilayani Kondoa.
Wakazi wa kata ya Mnenia iliyopo wilaya ya Kondoa wakisoma machapisho ya Sikika 
Mkazi wa wa wilaya ya Kondoa akisoma chapisho la Ripoti ya zoezi la SAM katika wilaya hiyo.

Mratibu wa kanda toka Sikika Bi. Norah Mchaki akizungumza na wakazi wa Mnenia wilayani Kondoa kuhusu umuhimu wa Haki ya Afya katika katiba mpya.

Nyumba ya Mganga mkuu katika Zahanati ya Chololo wilayani Kondoa.
Mratibu Sikika wilayani Kondoa Bw. Nelson Lema akizungumza na wakazi wa kijiji cha Chololo kuhusiana na hali ya upatikanaji wa huduma za afya  katika Zahanati ya kijiji hicho. 
Mratibu wa Sikika wilayani Kondoa Bw. Nelson Lema akichukua maelezo toka kwa wananchi wa Chololo kuhusiana na hali ya upatikanaji wa huduma za afya katika Zahanati ya kijiji hicho.


Wajumbe wa timu ya SAM wilayani Kondoa Bi. Joyce Ruta (kushoto) na Waziri Fataki wachukua amelezo juu ya upatikanaji wa huduma za afya katika Zahanati ya Chololo.
Mratibu wa Sikika wilayani Kondoa Bw. Nelson Lema akizungumza na wakazi wa kijiji cha Masawi kuhusu zoezi la SAM na upatijakanaji wa huduma za afya kijijini hapo. 
Wananchi wakiwa katika  kituo cha afya Mnenia wilayani Kondoa wakisubiri kufanya uchaguzi wa wawakilishi wa timu ya SAM.

Mratibu wa Sikika wilayani Kondoa Bw. Nelson Lema (aliyesimama katikakati) akizungumza na Wananchi (wapokea huduma za afya) katika Zahanati ya Thawi wilayani humo.



No comments: