Monday, August 4, 2014

Sikika yakanusha tuhuma za Madiwani, Halmashauri Kondoa: 03 Agosti, 2014

Mwenyekiti wa Bodi Sikika, Bi. Pili Mtambalike akisoma tamko la Sikika mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) kufuatia kusikitishwa na taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri wilayani Kondoa ya kusitisha shughuli zake katika wilaya ya Kondoa. Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika Bw. Irenei Kiria na Mjumbe wa Bodi ya Sikika Bw.Joseph Kamwihangiro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika Bw. Irenei Kiria akitoa ufafanuzi wa tamko lilisomwa mbele ya waandishi wa habari kufuatia kusikitishwa na taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri wilayani Kondoa ya kusitisha shughuli zake katika wilaya hiyo.   
Mwenyekiti wa Bodi Sikika, Bi. Pili Mtambalike akitoa ufafanuzi wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri wilayani Kondoa ya kusitisha shughuli zake katika wilaya hiyo. Kutoka kulia ni mjumbe wa bodi ya Sikika Dk. Elihuruma Nangawe na Kushoto ni Mjumbe wa Bodi hiyo Bw.Joseph Kamwihangiro.



 Mjumbe wa Bodi ya  Sikika Dk. Elihuruma Nangawe (Wapili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi wa tamko lilisomwa mbele ya waandishi wa habari kufuatia kusikitishwa na taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri wilayani Kondoa ya kusitisha shughuli zake katika wilaya hiyo.

  Mjumbe wa Bodi ya  Sikika Bw. Joseph Kamwihangiro (Wapili kushoto) akitoa maelezo juu ya tamko lilisomwa mbele ya waandishi wa habari kufuatia kusikitishwa na taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri wilayani Kondoa ya kusitisha shughuli za Sikika katika wilaya hiyo.

Mjumbe wa timu ya SAM Kondoa anayewakilisha makundi ya Dini Bw. Waziri Fataki (Kushoto) akitoa ufafanuzi wa tuhuma zilizotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri wilaya ya Kondoa kuwa Madiwani hawajasoma. 

Mwakilishi kutoka  Asasi zisizo za Kiserikali Bi. Salama Salumu (Kushoto) akitoa ufafanuzi wa baadhi ya tuhuma zilizotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri wilaya ya Kondoa kuwa Madiwani hawajasoma. 
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwajibika.

No comments: