Friday, June 12, 2015

Mdau wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Switzerland alipotembelea Wilayani Kibaha na Katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za Afya

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibaha, Bi. Tatu Selemani akiongea na timu ya Sikika pamoja na Mdau wa maendeleo kutoka ubalozi wa Switzerland - Tanzania, Bi. Aurelie Righetti, (Wa kwanza kutoka kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibaha, Bi. Tatu Selemani akiongelea juu ya upatikanaji wa huduma bora za Afya hasa kwa upande wa Madawa na Vifaa Tiba.


Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibaha, Bi. Tatu Selemani akikazia jambo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibaha, Bi. Tatu Selemani katika picha ya pamoja na timu ya Sikika pamoja na Mdau wa Maendeleo, Aurelie Righetti, (wa pili kutoka Kulia).
Afisa Tawala wa Wilaya ya Kibaha, Bi. Sozy Ngate (Wa pili kutoka kushoto), Bi Tatu Selemani na Mganga Mkuu wa Wilaya Bi. Mariam Malliwah (Wa kwanza kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Wadau kutoka Sikika.




Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi. Mariam Malliwah akimueleza jambo Afisa program - Idara ya Afya Bi. Aurelie Righetti. 
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi. Mariam Malliwah akieleza jambo.






Mwenyekiti wa timu ya SAM, Bi. Josephina Gunda akielezea juu ya mafanikio ya zoezi la SAM katika baadhi ya vituo vya Afya.
Bi. Josephina Gunda akisisitiza jambo.
Katibu wa timu ya SAM wilaya ya Kibaha Bw. Mfalamagoha akisoma ripoti fupi kuhusiana na upatikanaji wa huduma za afya katika wilaya hiyo. 



Wajumbe wa timu ya SAM wilayani Kibaha wakisikiliza kwa makini ripoti inayowasiliswa.
Mjumbe wa timu ya SAM akichangia jambo.


Timu ya SAM wilaya ya Kibaha katika picha ya pamoja na Wadau kutoka Sikika.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mlandizi Dkt. Adronicus Aloyce Rwelamila akieleza baadhi ya mafanikio katika katika kituo hicho yaliyotokana na timu ya SAM - Kibaha. 
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mlandizi Dkt. Adronicus Aloyce Rwelamila akisisitiza jambo.
Bi. Beatrice Mkani kutoka Sikika akichangia jambo.



Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mlandizi Dkt. Adronicus Aloyce Rwelamila katika picha ya pamoja. 
Dkt. Adronicus Aloyce Rwelamila akionesha upatikanaji wa taarifa katika ubao wa matangazo.
Baadhi ya wagonjwa wakisubiri kupatiwa matibabu katika kituo cha Afya Mlandizi. 
Gharama za uchangiaji wa huduma za Afya katika kituo cha afya Mlandizi kama zinavyooneka katika ubao.

Baadhi ya wagonjwa wakichukua Dawa katika dirisha la dawa kwa wagonjwa wa Bima (NHIF na CHF). 



Fomu anayopewa mgonjwa baada ya kuandikishwa kabla ya kumuona daktari, pia fomu hii huonyesha kama mgonjwa ni mwananchama wa CHF, NHIF au wa malipo ya papo kwa papo.
Jengo la kupumzika wagonjwa.
Moja ya jengo la wagonjwa wa nje (OCD) katika kituo cha afya Mlandizi.
Mtendaji wa kata ya Soga Bw. Mfalamagoha akielezea juu ya upatikanaji wa huduma za afya katika Zahanati ya Soga wilayani Kibaha. 
Mganga Mfawidhi katika Zahati ya Soga, Bi. Husna Ngunga akielezea mafanikio walioyapata juu ya wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya nchini (CHF).



Muuguzi katika Zahanati ya Soga akionesha stoo ya dawa.
Mgawanyo wa fedha za CHF kama unavyoonekana katika picha. 
Watoa huduma katika Zahanati ya Soga na Wadau kutoka Sikika.

Zahanati ya Soga.

No comments: