Tuesday, October 20, 2015

Uzinduzi wa Tuzo ya Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015, makampuni mawili yaongezwa

Mshindi wa tuzo ya umahiri EJAT 2014 ya mpiga picha bora wa mwaka kutoka Gazeti la Mtanzania Abubakari Akida akielezea jinsi alivyoshiriki katika tuzo za CNN na kuibuka mshindi wa pili. 

Mshindi wa tuzo  za umahiri EJAT 2014 (Habari za Elimu na Jinsia kwa upande wa magazeti), Bw. Richard Makore kutoka gazeti la Nipashe akiwaasa waandishi wenzake jinsi ya kuandika habari za kiuchunguzi na kutumia chanzo zaidi ya kimoja



Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka PPRA, Mcharo Mrutu akieleza ushiriki wao katika tuzo za EJAT kwa mara ya kwanza kupitia kigezo cha  habari za manunuzi ya umma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania 2015  kwa awamu ya saba. Kwa  mwaka 2015 vigezo vipya  mawili vimeongzeka ambayo ni habari za kodi na za manunuzi ya umma, hivyo kufanya kuwe na makundi 22 vya kushindaniwa. 
 Bw. Kajubi Mukajanga akisisitiza jambo. Kutoka (Kushoto) ni Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano kutoka Sikika Bi. Lilian Kallaghe.
Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia uzinduzi huo kwa makini. 



Mtangazaji wa East Africa radio, Steven Mumbi akiuliza swali katika mkutano huo. 


Jaji mkuu katika tuzo za EJAT 2014 Bw. Chrysostom Rweyemamu akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari. 

Bw. Chrysostom Rweyemamu akisisitiza waandishi kuandika habari  kwa kuzingatia usahihi wa taarifa pamoja na kutumia chanzo cha habari zaidi ya kimoja.  Kutoka (kushoto) ni Mkurugenzi wa TAMWA Bi. Edda Sanga.
Bi. Pili Mtambalike (Kulia) kutoka MCT akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari juu ya tuzo za EJAT. Kushoto ni Mkuu wa kutengo cha Habari na Mawasiliano kutoka Sikika Bi. Lilian Kallaghe.  


Mshindi wa tuzo ya umahiri  EJAT 2014 ya  mpiga picha bora wa mwaka kutoka Gazeti la Mtanzania Abubakari Akida akionesha tuzo yake aliopata toka CCN. 

No comments: