Tuesday, May 17, 2016

USIKU WA TUZO ZA UMAHIRI WA UANDISHI WA HABARI ZA EJAT 2015

Mkurungenzi wa Sikika Bw. Irenei Kiria akimkabidhi tuzo Joseph Mwendapole kutoka Gazeti la Nipashe baada ya kuibuka mshindi kwenye Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari za EJAT 2015, katika kuripoti habari za afya (Health Reporting) kwa upande wa Magazeti. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam.



Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, ambaye pia ni mgeni rasmi katika hafla hiyo Mh.  Bahame Nyanduga akimkabithi cheti cha ushiriki Bw. Irenei Kiria. (kushoto) ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga.
 Saidi Michael (Wakudata) mchora katuni kutoka Gazeti la Mtanzania akionesha tuzo yake baada ya kuibuka mshindi katika kipengele cha Mchora Katuni bora katika Tuzo za Umahiri za EJAT 2015.
 Mh.  Bahame Nyanduga akimkabithi mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh. Milioni 3 mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Frank Bahati baada ya kuibuka mshindi wa jumla kwenye Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari za EJAT 2015. Kulia ni
Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo.
Mshindi wa jumla kwenye Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari za (EJAT 2015) Bw. Frank Bahati akihojiwa.

Kikundi cha ngoma kikitoa burudani.
Mwenyekiti Mtendaji wa  IPP Bw. Reginald Mengi (Wapili kulia) akiwa na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (Katikati) na Mh.  Bahame Nyanduga (kushoto) wakifurahia jambo wakati hafla hiyo.
Wadau kutoka mashirika mbalimbali nchini walioshiriki katika usiku wa Tuzo za EJAT 2015.
Bw. Kajubi Mukajanga (Kushoto) akijadili jambo na mgeni rasmi Mh. Bahame Nyanduga.
Mlimiki wa Kituo cha Radio cha ABM kilichopo Mjini Dodoma Bw. Abdallah Majura (Kulia) akiwa na baadhi ya wadau wengine waliohudhuria utaoji wa tuzo hizo.



Bi. Rose Haji Mwalimu akilia baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika tuzo ya maisha ya mafanikio katika uandishi wa habari (EJAT 2015). 

Mh. Bahame Nyanduga akimkabithi tuzo Bi. Rose Haji Mwalimu baada ya kuibuka mshindi katika tuzo ya maisha ya mafanikio katika uandishi wa habari (EJAT 2015). 




Washindi wa Tuzo za EJAT 2015 katika picha ya pamoja.

No comments: