Wednesday, March 23, 2016

Sikika yajadiliana na Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii

Sikika ilifanya mjadala na Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, jana tarehe 22 Machi, 2016  na kuzungumzia changamoto za Kisera, Bajeti na Utekelezaji  wa huduma za Afya nchini.



Kamati hiyo ya Bunge iliomba kukutana na Sikika kufuatia tamko la Shirika kuhusu kuishauri serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha hatua za mwanzo za uandaaji wa bajeti za serikali unakua na umakini mkubwa ili kuepuka kusababisha mianya inayoweza kupelekea bajeti kuwa na matumizi yasiyo ya lazima yanayoweza kusababisha ufujaji wa fedha za umma.



Lengo la kamati hii ya bunge kutaka kukutana na wadau wa sekta ya afya ni kupata uzoefu na uelewa zaidi kabla ya kukutana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Mh. Ummy Mwalimu.



Kati ya mambo makuu yaliyojadiliwa ni: Utendaji kazi wa Sikika, Sekta ya Afya na changamoto zake, pamoja na mfumo wa Mgawanyo wa Bajeti.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Dk. Raphael Chegeni akifungua mjadala kati ya Sikika na kamati hiyo ya Bunge. (Pembeni yake ni Katibu wa kamati hiyo  ya Bunge).
 
  Dk. Raphael Chegeni akionyesha gazeti lililoituhumu kamati hiyo kwa ufisadi.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Bw. Irenei Kiria akielezea Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii juu ya Shirika na namna linavyofanya kazi katika sekta ya afya nchini ili kutetea upatikanaji wa huduma bora za Afya kwa kila mtu. 


Mkuu wa Idara ya  Dawa na Vifaa Tiba wa  shirika la Sikika, Bi. Alice Monyo akielezea juu ya umuhimu wa sekta ya afya na changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta hiyo. 


 Dk. Wilson Kitinya kutoka Sikika akitoa mada juu ya mfumo wa mgawanyo wa bajeti.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati kuanzia kushoto Mh. Dr. Charles Tzeba (CCM-Buchosa), Mh. Juma Nkamia (CCM-Kondoa), Kabwe Zuberi Zitto (ACT-Kigoma Mjini) wakifuatilia mjadala.
Mh. Kabwe Zuberi Zitto akichangia mada. 
Mh. Dr. Charles Tzeba akiuliza swali juu ya mgawanyo wa watumishi wa afya nchini,
mojawapo likiwa ni kutaka kujua kwanini watumishi wa afya wapo wengi Kinondoni lakini hawapo Singida...?

Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Jacqueline Kandidus Ngonyani (CCM) akichangia  jambo.
 
Mbunge wa Buyungu  Mhe. Kasuku Samson Bilango (CCM) akielezea kwa uchungu vifo vya mama wajawazito pamoja na kukosekana  kwa magari ya huduma za wagonjwa (ambulance).
Mh. Juma Nkamia (CCM-Chemba) akiuliza maswali juu ya shirika la Sikika kuwa  lina bajeti kiasi gani, linapata wapi pesa ya kujiendesha, wafadhili wake ni wakina nani na kama shirika linafanya ukaguzi wa mahesabu.
Mbunge wa Nzega (CCM) Mh. Hussein Bashe akiuliza maswali, mojawapo likiwa ni kutaka kujua kama Sikika huwa inafuatilia iwapo dawa zinazoandikwa kupelekwa katika vituo vya afya huwa zinafikishwa eneo husika au la kutokana na tatizo sugu la kukosekana kwa dawa katika vituo vya afya.
Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Susan Anselm Jerome (Chadema) akifuatilia mjadala kati ya Sikika na kamati ya bunge wakifuatilia mjadala.  
Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia mjadala.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Sikika akijibu swali la mjumbe wa Kamati Mh. Juma Nkamia  (wa kwanza kulia) juu ya shirika la Sikika kuwa  lina bajeti kiasi gani, linapata wapi pesa ya kujiendesha, wafadhili wake ni wakina nani na kama shirika linafanya ukaguzi wa mahesabu.
 Mkuu wa Idara za Sikika  Bw. Patrick Kinemo akielezea sababu mbalimbali zinazosababisha vifo vya akina mama na watoto. 

Dk. Wilson Kitinya kutoka Sikika akifafanua jambo katika mkutano huo.


No comments: