Thursday, June 19, 2014

Zoezi la Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) laanza kwenye wilaya za Singida na Mpwapwa kwa mwaka 2014

 Mwezeshaji toka Sikika Bw. Jackson Sikahanga akiendesha Mafunzo ya SAM katika wilaya ya Mpwapwa.

Baadhi ya wajumbe wa timu ya SAM wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini, wa kwanza toka (kushoto) ni Bw. Nestory Ngunwa, (katikati) Bw. Michael Kuchela (kulia) na Bw. Yohana Madinda wilayani Mpwapwa.

Bw. Yohana Madinda toka (kushoto) na Bi. Zeli Mtula wakifuatilia mafunzo hayo.


Baadhi ya wajumbe wa timu ya SAM wakifuatilia mafunzo hayo kwa umakini toka (kulia) ni Bw. John Mwilongo, (katikati) Bi. Victoria Chizua na Bi. Pamela Mnemele (kushoto).


Bw. Michael Kuchela,  akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.

 Afisa Mtendaji wa kata Mpwapwa mjini Bi. Gift Ngatunga akitoa maelezo
katika mafunzo hayo.


Wajumbe wa timu ya SAM wilayani Mpwapwa wakifuatilia mafunzo hayo.






Bi. Norah Mchaki toka Sikika ambaye pia ni mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo ya SAM akitoa mafunzo hayo kwa timu ya SAM wilayani Singida vijijini.
 Bw. Ramadhani Hamisi ambaye ni mmoja wa washiriki wa mafunzo ya SAM akielezea washiriki wenzake kazi iliyofanyika katika kikundi chao wilayani Singida.

Washiriki wa mafunzo ya SAM wakiwa darasani katika mafunzo ya SAM 2014 katika wilaya Singida vijijini.
Mshiriki wa mafunzo ya SAM Bi. Veronica Mure akichangia jambo wakati wa mafunzo hayo wilayani humo.

No comments: