Tuesday, February 9, 2016

Madiwani wairudisha Sikika wilayani Kondoa

Wiki iliyopita (04 Februari, 2016) Sikika ilialikwa katika kikao cha Baraza la Madiwani Wilayani Kondoa kwa lengo la kufanya uamuzi wa kuliruhusu  shirika hilo kufanya kazi zake kama ilivyokuwa awali. Mwezi Juni, 2014 Baraza lililopita liliipiga marufuku taasisi hiyo kufanya kazi katika wilaya hiyo baada ya kutoa ripoti ilioonyesha upungufu katika utoaji wa huduma za afya unaofanywa na watendaji wa Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mh. Omari Kariati akiingia katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 4, mwaka huu wilayani humo. Katika kikao hicho baraza hilo liliazimia kwa pamoja kutengua uamuzi wake wa kuifukuza  taasisi ya Sikika kufanya kazi ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii katika sekta ya afya (SAM).


Mh. Omari Kariati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani, kulia ni Mwanyekiti Msaidizi Mh. Hija Sulu na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Hussein Ngaga Issa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika Bw. Irenei Kiria akijitambulisha mbele ya baraza la Madiwani.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Chiku Gallawa akitoa hotuba katika kikao hicho na kuwapongeza madiwani kwa kuiruhusu Sikika kufanya kazi katika Wilayani humo. Pia aliwasihi madiwani ikiwezekana kuruhusu na taasisi zingine kufanya kazi kama wanahitaji maendeleo ya kweli hasa uwazi katika utoaji huduma za jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bw. Shaaban Kissu (Kulia) na Mwenyekiti Msaidizi wa Halmshauri hiyo Mh. Hija Sulu.
Baadhi ya Madiwani wakipitia makabrasha na kufuatilia taarifa zinatolewa katika kikao cha baraza hilo.







Mwanasheria wa Halamshauri ya Kondoa Bw. George Makacha (wa kwanza kushoto) akifuatilia mjadala.





Mh. Khadija Kilala (Diwani) akichangia jambo katika kikao cha baraza la hilo.
Bw. Irenei Kiria akipongeza uamuzi wa Madiwani kwa kutambua umuhimu wa Sikika katika halmashauri hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano kwao.

Mh. Omari Kariati akiwashukuru Madiwani kwa kuirudisha Sikika na kusema uamuzi huo umezingatia maslahi ya wananchi wa Kondoa.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifanya mahojiano na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bw. Shaaban Kissu.
Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifanya mahojiano na Madiwani. 



No comments: