Thursday, February 11, 2016

Sikika yashiriki Mkutano wa 16 wa Mwaka wa Mapitio ya Sekta ya Afya, Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa nne wa Sekta ya Afya 2015-2020

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akifungua mkutano wa 16 wa mwaka wa mapitio ya Sekta ya Afya. Kulia ni Carol Hannon Mshauri wa Afya katika ubalozi wa Ireland nchini Tanzania.
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI - Afya, Dk. Deo Mtasiwa akitoa hotuba fupi katika mkutano huo.

Mkurugenzi wa Sikika Bw. Irenei Kiria akisoma hotuba kwa niaba ya Asasi za Kiraia nchini.

Mkurugenzi utoaji Huduma za Afya Bi. Josephine Bulati akisoma hotuba kwa niaba ya Sekta binafsi na Mashirika ya Dini.
Wadau mbalimbali katika Sekta ya Afya wakifuatilia majadiliano.




Mkuu wa Idara ya Dawa na Vifaa Tiba (Sikika) Bi. Alice Monyo (wa kwanza kushoto) akichangia mada.

Mkurugenzi wa sekta binafsi katika masuala ya Afya, Dr. Samwel Ogillo akichangia mada katika mkutano wa mapitio ya sekta ya afya.
 Mh. Ummy Mwalimu akielezea vipaumbele nane vya Sekta ya Afya kwa mwaka 2016/2017.


Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Selemani Jafo akielezea juu ya ufungaji wa mashine za kielektroniki ili kuongeza mapato katika vituo vya Afya nchini.
 Mh. Ummy Mwalimu (katikati) akizindua Mpango Mkakati wa Nne wa Sekta ya Afya 2015 - 2020 (HSSP IV).




 Bw. Irenei Kiria (kulia) akikabidhiwa Mpango Mkakati wa Nne wa Sekta ya Afya 2015-2020 (HSSP IV) kwa niaba ya Asasi za Kiraia nchini na Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu.




Mh. Ummy Mwalimu akitoa maelezo baada ya uzinduzi wa mpango huo.
 Bw. Irenei Kiria akichangia mada kuhusu HSSP IV.
Picha ya pamoja: Mh. Ummy Mwalimu (wa nne kutoka kushoto) akiwa na Wadau wa Sekta ya Afya.


Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Bw. Irenei Kiria akifanya mahojiano na Waandishi  wa Habari nchini juu ya mkakati mpya wa Afya.


Bw. Irenei akisalimiana na Mr. Konga kutoka Wizara ya Afya. 
  
Pia unaweza kupata tamko la Asasi za Kiraia kupitia www.sikika.or.tz
 

No comments: